Jumatatu 25 Mei 2026 - 07:30
Vita vyovyote dhidi ya Iran vitakuwa vita vya kikanda na vya nyanja nyingi

Hawza/ Muhammad Ali Al-Hakim, mchambuzi wa kisiasa wa Iraq, amesema kuwa; vitisho vya Donald Trump Rais wa Marekani, vinafanywa kwa lengo la kuilazimisha Iran kupatana na kufanya makubaliano ya kuondosha baadhi ya misimamo yake.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tajrama cha Shirika la Habari la Hawza, Muhammad Ali Al-Hakim, mchambuzi wa kisiasa wa Iraq, akieleza kwamba vitisho vya Donald Trump, Rais wa Marekani, vinalenga kuilazimisha Iran kutoa mapatano, alibainisha kuwa makabiliano yoyote ya kijeshi yanayoweza kutokea hayatakuwa vita vifupi, bali vitakuwa vita vya kikanda na vya nyanja nyingi.

Al-Hakim alisema: “Vitisho vya Donald Trump dhidi ya Iran, zaidi ya kuwa tangazo la moja kwa moja la vita vinavyokaribia kutokea, mara nyingi hutumiwa kama chombo cha shinikizo la kisiasa na mbinu ya kimkakati ya kuzuia na kuutisha upande mwingine, hasa kwa kuzingatia kwamba matamshi hayo ya uchochezi yanafuatwa kwa lengo la kuilazimisha Tehran kukubaliana katika suala la nyuklia na kupunguza ushawishi wake wa kikanda.”

Aliongeza kuwa: “Washington inafahamu vizuri kwamba; makabiliano yoyote na Iran hayatakuwa vita vya kawaida na vifupi, bali utakuwa mzozo wa kikanda na wa nyanja nyingi ambao utahusisha eneo lote kuanzia Ghuba ya Uajemi hadi nchi zote za eneo hili, aidha vitisho vya Marekani vina vipengele vya kijeshi, lakini wakati huo huo vina athari na malengo ya kisaikolojia na kiuchumi.”

Mchambuzi huyu wa kisiasa alisisitiza kuwa: “Makabiliano yoyote ya moja kwa moja ya kijeshi dhidi ya Iran yatabeba gharama kubwa sana za kiuchumi na kiusalama kwa Marekani na washirika wake katika eneo hili.”

Al-Hakim alisema: “Washington inafahamu kwamba Iran, kupitia washirika wake wa kikanda na uwezo wake wa makombora, inamiliki nyenzo za kujibu kwa mbinu zisizo za kawaida za kivita. Zaidi ya hayo, taasisi ya kijeshi ya Marekani inajua kwamba; huenda shambulio la kwanza likawa rahisi kutekeleza, lakini kudhibiti matokeo na athari zake kutakuwa jambo gumu sana na lenye gharama kubwa.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha